Pudini (Pudding) Ya Mayai
VIPIMO
1) maziwa 2 ½ mugs
2) mayai 8
3) sukari 1 kikombe cha chai
4) hiliki ½ kijiko cha chai
JINSI YA KUIPIKA PUDDING
1) Unatia mayai yote 8 kwenye blender,maziwa ,hiliki na sukari robo kikombe ikisha unasaga kwa dakika 3.
2)
Sukari iliyobaki unaitia kwenye sufuria moto mdogo mdogo unaiyayusha
mpaka iyayuke na iwe brown,unaiwacha kidogo ikisha unaisambaza kwenye
sufuria humo humo. Mpaka ienee nusu ya sufuria lako.
3) Chukuwa mchanganyiko wa maziwa na mayai umimine humo kwenye sufuria la sukari iliyoyayushwa halafu funika.
4)
Chukuwa sufuria nyingine kubwa ya hiyo uliyotilia sukari na
mchanganyiko ikisha itie maji nusu na uiteleke ndani yake tia sufuria
yako yenye pudding.kumbuka sufuria ya pudding itakuwa inaelea kwahiyo
tafute kitu kizoto ukiweke juu ya sufuria ya ndani yenye pudding.
5)
Iache itokote mpaka maji yakianza kumalizika ongeza maji mengine ,huku
unaifunguwa kuitizama ukiona tayari imeshaganda yaani imeshajishika basi
iepuwe wacha ipowe.
6) Ikipowa mimina kwenye chombo kama sahani yenye shimo kidogo ikisha weka ndani ya fridge, ikishapata ubaridi tayari kwa kuliwa.
No comments:
Post a Comment