Ndugu
zangu watanzania, chuo cha Westminster kilichopo katikati ya jiji la
london, UK, kila mwaka kinatoa scholarship kwa watanzania kusoma degree
ya kwanza na ya pili bure (unalipiwa ndege kwenda london na kurudi
Tanzania, maradhi, chakula, ada yote na kila mwezi hela ya matumizi).
Tatizo hizi habari tukipata hatupeani, mwisho nafasi kama hizi zinafutwa
chuoni maana hamna wanaoziomba. Mi nilifanikiwa kuipata kupitia rafiki
yangu, nami nimekuwa naitangaza na ntaendelea. Hii nafasi itasaidia
kubadilisha maendeleo ya watanzania na Maisha yao kiujumla. Link hiyo
chini inamaelezo yoote. Deadline ni mwakani April, so kama upo
interested, tumia mda huu kudownload form za kuomba chuo, ukipata chuo,
then unaomba scholarship, maelezo yapo kwenye website yao www.westminster.ac.uk link ni http://2009.westminster.ac.uk/study/international/country-pages/africa/tanzania
Goodluck
Evelyn Kaijage
"Asante sana Evelyn kwa kutuhabarisha maana si wengi wenye moyo kama huu. Mungu akubariki."
TAFADHALI MJULISHE NA MWENZIO UONAPO HABARI HII!
Asanteni sana
No comments:
Post a Comment