SALADI YA MAHINDI
Vipimo
Majani ya saladi (lettuce) ½ msongo
Kabeji ya Zambarau ¼
Mahindi 1 kikombe
Tango 1
Kitunguu majani (spring onion) 3
Nyanya 2
Salsali (salad dressing)
Thomu iliyosagwa 2 chembe
Chumvi kiasi
Ndimu au siki 2 jiko vya supu
Mafuta ya zaytuuni ¼ kikombe
Pilipili ya unga nyekundu ½ kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha
- Katakata majani ya saladi, kabeji, weka katika bakuli.
- Menya tango, katakata tia pamoja.
- Chemsha mahindi au tumia ya tayari ya kopo, mwaga maji.
- Katakata kitunguu majani, nyanya.
- Changanya vitu vyote pamoja.
- Tayarisha Salsali yake kwa kuchanganya vitu vyote, weka kando hadi wakati wa kula umwagie juu yake na uchanganye vizuri.
No comments:
Post a Comment