SHUKRANI ZA DHATI KUTOKA
WATANZANIA WA NJE YA NCHI KWA RAIS
JAKAYA KIKWETE NA SERIKALI YAKE YA AWAMU YA NNE.
Naomba kuchukua fursa hii
kutoa shukrani za dhati na wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Kikwete na Serikali yake ya awamu ya nne, kwa niaba yangu binafsi na kwa
niaba yaTawi la CCM UK na nina imani kwa niaba ya wana jamii ya Wa-Tanzania
Walioko Nje ya Nchi (Dispora) kwa
Ujumla, katika juhudi anazofanya kujumuisha Dispora Tanzania kwenye kuchangia
maendeleao ya Nchi yetu.
Wana-Dispora tulio wengi
tumeshuhudia kwa vitendo
tangu Rais Jakaya Kikwete na
Serikali yake imeingia Madarakani , jitihada
na mikakati tofauti na iliyo wazi
ya Serikali Kuu kutafuta mbinu za
kudumu ili kushirikiana na kuwahusisha wana Diaspora, katika kuchangia
maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii ya Nyumbani, Tanzania.
Nakumbuka Mheshimiwa Rais
Kikwete katika kikao chake cha kwanza na Watanzania waishio Uingereza Mnamo
mwaka wa fedha 2006/2007 pale Churchill
Hotel, UK , katika Hotuba yake ambayo mbali na kutuelezea mafanikio na mikakati
mbalimbali iliyopangwa na serikali yake kwenye utekelezaji wa Sera zake za Serikali
ya awamu ya nne, kwa nia ya kutimiza
maazimio ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2005 na baadae 2010, vile vile alituahidi
wana-Dispora kuwa atahakikisha yeye Binafsi atafanya jitihada zake zote kwa
kadri ya uwezo wake aliyopewa na Mwenyezi Mungu
na Serikali yake haitusahau na katuacha nyuma Wana-Dispora .
Kilichoendelea baada ya Mkutano ule wana Dispora UK tulishudia thamani yetu kwa
Serikali na Taifa letu ,kwani tumekuwa tukipewa kipaumbele kwa kila Kiongozi
Mkuu wakiwemo Mawaziri na Wabunge wetu tofauti,
wanapotembelea Uingereza (na nina
imani Nchi nyingine mbalimbali ) mbali na kuwa na ratiba zao ndefu za kikazi, wanapata muda wa kubadilishana mawazo nasi na tunaona
matunda ya mchango wetu yameanza kuonekana ,licha ya kuwepo changamoto za
kawaida zinazokabilika. Hili tunamshukuru sana Rais wetu kwa kulipa uzito
unaostahili na kuonyesha mfano wa Uongozi wake bora na uliotukuka.
Kwa mara ya kwanza Tanzania
Dispora tumepata sauti na kuthaminiwa
kwa wazi kwa Mchango wetu wa hali na
mali tunaorudisha nyumbani ili kuchangia Maendeleo ya Nchi. Wana-Dispora
sasa tunajivunia kupewa na Rais
wetu jina la Mkoa . Baada ya kuanza na
dawati la Dispora pale Wizara ya Mambo ya Nje, ili kuweka mfumo wa kudumu na
kutimiza ahadi yake Mheshimiwa Rais mwaka ulipita 2012 aliteua Mkurugenzi wa
Idara ya Dispora. Sasa tuna Idara/Kitengo kizima na si dawati tena. Kitengo/Idara
yenye jukumu la kushughulikia mambo muhimu na tofauti ya Dispora. Hii ni hatua
kubwa sana na ya muhimu na hatutaacha kumshukuru Rais wetu kwa kuliona na
kulitambua hili na kutuletea matunda yake.
Licha ya yote hayo ya
kiutendaji yanayoendelea, na jambo kubwa lililofanya kuandika shukrani hizi za
dhati na za wazi ni kilichotendeka wiki iliyopita kupitia vyombo vya habari na
Blogu za jamii tumeshuhudia tukio la kihistoria pale ambapo Rais Jakaya
Kikwete, Chini ya Ofisi yake Ikulu , wametoa fursa kwa Wa-Tanzania Wataalamu
waliopo Nje na Ndani ya Nchi kupeleka
wasifu wao (CV) moja kwa moja Ofisi za Katibu Mkuu Kiongozi -Ikulu, ili tuweze kupata nafasi za kazi kuchangia
moja kwa moja na kuwa mstari wa mbele kuijenga nchi yetu . Hiki kimekuwa kilio
cha muda mrefu cha Watanzania (na hususan Wana-Dispora) kuomba serikali kutumia
zaidi wataalamu wa kitanzania na si wa kigeni , na tumefurahi sana kuwa Serikali yetu kwa mara
ya kwanza na kwa uwazi kabisa
imetusikiliza kwa hili .
Naomba kutoa wito na shime kwa
WaTanzania wote waliopo nchi mbalimbali duniani
, ni wakati umefika sasa Nchi yetu
inatuhitaji na Serikali yetu imetupa nafasi hii adhimu basi na tujipange na
tujitokeze kwa wingi ili tuweze kwenda nyumbani kuchangia maendeleo ya Tanzania
yetu katika nyanja tofauti na kwa kadri ya uwezo wetu na kwa yale mazuri
tuliyojifunza Ughaibuni.
naomba kumalizia kwa ule usemi usemao kuwa
"Asiyemshukuru Binadamu mwenzie basi hata Mwenyezi Mungu hawezi kumshukuru
" na kwa mantiki hiyo, kwa heshima kubwa Naomba kutanguliza shukrani zangu
za dhati kwa mpendwa Rais wetu Jakaya
Mrisho Kikwete kwa kujitolea kwake na kufanya kazi ngumu mno ya kuliongoza
Taifa letu na nakumuombea kwa Mwenyezi Mungu yeye Binafsi na Viongozi wetu wote afya njema na
hekima za kuweza kupambana na majukumu yao ya kila siku .
Kwa Wana -Dispora Wenzangu
popote pale mlipo Duniani , ngoma iko uwanjani na tuicheze sasa, CV
zinahitajika .........haya mama
Harambeeeee
Mugu Ibariki Afrika, Mungu
Ibariki Tanzania
Umoja Ni Ushindi .
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Mariam Mungula
Katibu wa CCM - Uingereza