Pages

Ads 468x60px

Sunday 26 August 2012

KONA YA MAPISHI


SAMBUSA ZA VIAZI

 undefined
Vipimo
Viazi                                                                          4
Vitunguu nyasi vilokatwakatwa                                    3 miche
Kitunguu maji kilokatwakatwa                                     1
Chumvi                                                                     1 kijiko cha chai
Bizari ya pilau nzima ( jeera)                                      1 kijiko cha chai
Mafuta                                                                       Nusu kilo
Manda za tayari                                                         10 - 20                                
Yai                                                                            1 au 2
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Menya viazi, vioshe vikate slesi kisha  vikatekate vipande vidogo vidogo.
    
  1. Chemsha maji kidogo ukiwa umeyatia chumvi , kisha vimimine viazi ndani ya maji yawache paka uwone tena yachemka kwa mara ya pili acha kwa dakika 10 - 15, kisha ondoa jikoni.
  1. Mimina katika chujio uchuje maji .
  1. Roweka bizari kwenye maji kwa muda wa dakika 20 hivi.
  1. Chukua bakuli kubwa lenye nafasi mimina viazi, vtunguu nyasi na maji,   chumvi, mafuta vijiko 2 3 vya supu, na bizari. Changanya vizuri.
  1. Tandaza manda mezani au kwenye kibao fanya mkunjo wa sambusa kisha paka yai kwa brashi, kunja upate pembe moja . Tazama picha.
     
  1. Jaza viazi sehemu ulokunja kisha funga sambusa.
               
  1. Tia mafuta katika karai, yakipata moto, tia sambusa ziikaange hadi zigeuke rangi ya dhahabu.  
  1. Zitoe na zichuje mafuta tayari kuliwa kwa Sosi Ya Ukwaju  au  Chatine Ya Mtindi

Wednesday 8 August 2012

TAWI LA CHADEMA LONDON LAZINDULIWA NA VIONGOZI WA MPITO WACHAGULIWA

 Kamanda Godbless Lema akiongea machache wakati wa uzinduzi wa tawi la CHADEMA jijini London nchini Uingereza
 Mwenyekiti wa tawi la Chadema London Kamanda Chris Lukosi akimwaga sera zake wakati wa    uzinduzi huo
                       Kamanda Dr Alex ambae ni mweka hazina akimwaga sera zake
                                   Makamu mwenyekiti Liberatus akichukua minutes
                                    Katibu wa vijana Emanuel Lunyama akimwaga sera
 Jessica Maduhu mwenyekiti wa baraza la wanawake CHADEMA tawi la London akimwaga sera
Margareth katibu wa wanawake CHADEMA tawi la London akiongea machache

Kwa habari zaidi www.jestin-george.com