Pages

Ads 468x60px

Tuesday, 3 January 2012

KONA YA MAPISHI

Nyama Ya Kukaanga Na Mboga Ya Mchicha (Spinach)

 Vipimo:
Nyama isiyo na mifupa                                 1 Ratili (LB)
Thomu na tangawizi iliyosagwa                       1 Kijiko cha supu
Kitunguu                                                        1 kikubwa
Pilipili manga ya unga                                       1/2-1 Kijiko cha chai
Bizari ya unga(Garam masala)                        1 Kijiko cha chai
Chumvi                                                           Kiasi
Sosi ya soya(soy sauce)                                 2 Vijiko vya supu
Mboga(Spinach) ya barafu iliyokatwa               1 pakiti
Hummus(Chick peas)                                     1 Kopo
Mafuta ya kukaangia                                       1/4 kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1.      Katakata nyama vipande vidogo. 
2.      Weka mafuta katika sufuria na kaanga kitunguu hadi iwe rangi ya brauni.
3.      Kisha kaanga thomu na tangawizi na vyote vilivyo baki ,pamoja na nyama isipokuwa spinach na hummus.
4.      Nyama ikishakuwa si nyekundu tena, weka maji kiasi ya kuiivisha.
5.      Nyama ikishaiva na karibu kukauka, tia hummus na spinach na iwache dakika chache.
6.      Epua na tayari kuliwa na wali.

 

2 comments:

Anonymous said...

Kuna haja gani ya kurudia mapishi ya alhidaaya kwenye blog yako?

Anonymous said...

Humus ndio nini? tafadhali nijuze please