Pages

Ads 468x60px

Monday, 30 January 2012

KONA YA MAPISHI

DESERA (WAFFLES)
 
Mahitaji:


1. Blue Band 1/4kg

2. Sukari Kopo moja la Blue Band 1/4 mpaka kwenye mstari wa chini pale kwenye kopo

3. Unga Ngano kopo2 blue band 1/4kg jaza mpaka juu usifanye mlima

4. Maziwa fresh kopo moja la blue band 1/4kg yafike chini ya mstari

5. Mayai 6


6. Baking Powder vijiko 2 vya chai jaza sana


7. Vanilla vifuniko 2 vya kale kachupa kadogo

UANDAAJI:
1. Changanya blue band yote na sukari ponda mpaka vilainike kabisa kusiwe na chengachenga za sukari

2. Weka mayai yote 6 ktk mchanganyiko wakwanza changanya mpaka vichanganyike vizuri

3. Weka ngano kopo zote 2 ktk mchanganyiko huo, changanya mpaka vilainike kabisa kusiwe na madongedonge

4. Weka maziwa yako changanya vizuri

5. Weka baking powder yako yote vijiko 2 changaya

6. Weka vanilla au esens yoyote uipendayo eg iliki, strawberr, rose etc. Changanya vizuri tayari kwa kupikwa

7. Kuna chuma chake spesho cha kupikia. Unaanza kuchoma. Ukimaliza ndo zinakua na muonekano huo kwenye picha. Ukichoma acha iwe brown. Unaweza kula na chai au juice.

No comments: