Pages

Ads 468x60px

Thursday 12 January 2012

KONA YA MAPISHI

CHAPATI ZA KUKU

VIPIMO
 Kuku wa kusaga 1lb

Nyanya 1 ndogo

Thomu 1½ kijiko cha chai

Tangawizi 1 kijiko cha chai

Pilipili manga 1 kijiko cha chai

Bizari unataka ½ kijiko cha chai

Kidonge cha supu 1

Pilipili mbichi 1 au 2

Chumvi kiasi

Vitunguu vya majani kiasi

Vitunguu 2

Mayai 6

Manda za tayari (spring rolls) 12

NAMNA YA KUTAYARISHA
 1. Saga nyanya, thomu, tangawizi na pilipili kwenye blender

2. Tia kima, vitu ulivyosaga, pilipili manga,kidonge cha supu, chumvi na bizari.

3. Weka motoni huku ukichanganya mpaka ikauke.

4. Kisha iache pembeni ipoe.

5. Kisha kata kata vitungu Kama vya sambusa na vitungu vya majani.

6. Chukuwa bakuli tia kima kama vijiko 4 au zaidi vya supu

7. Tia vitunguu vyote aina mbili kiasi na mayai mawili.

8. Chukuwa sinia ya oveni tia mafuta kama vijiko 2 au zaidi kidogo

9. Kisha panga manda 2 kwenye sinia.

10. Changanya mchanganyiko kwenye bakuli mimina juu ya manda utandaze.

11. Kisha funika manda 2 nyingine kwa juu na waweza kufanya 3 kwa pamoja.

12. Choma kwenye oveni moto wa chini ikishaiva tia mafuta geuza upande wa pili epua na itakuwa tayari kuliwa.

No comments: