Pages

Ads 468x60px

Monday, 6 August 2012

KONA YA MAPISHI


Mchuzi Wa Kuku Wa Nazi Na Mayai Ya Kuchemsha


Vipimo
Kuku 2 Lb (ratili)
Thomu na tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Bizari ya pilau ya unga ½ kijiko cha chai
Ndimu 1 kamua maji
Chumvi kiasi
Bizari manjano ½ kijiko cha chai
Vitunguu maji 1
Nyanya 2
Tuwi la nazi zito 1 ½ kikombe
Mayai ya kuchemsha 6

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Mchemshe kuku na thomu na tangawizi na ndimu na chumvi mpaka akauke.
  2. Saga vitunguu na nyanya kidogo tu kwa kutumia tui kidogo katika mashine (blender).
  3. Mimina kwenye kuku pamoja na bizari zote.
  4. Acha achemke kisha tia tui lichemke mpaka liwe zito
  5. Tia mayai ya kuchemsha.
  6. Pakua kwenye bakuli tayari kuliwa na wali au mkate. 

No comments: