Pages

Ads 468x60px

Thursday 22 December 2011

MAFURIKO MAFURIKO .............. DAR ES SALAAM

Diys Blog inatoa pole kwa familia za watanzania 13 waliopeteza maisha yao katika mafuriko makubwa yaliotokana na mvua ambazo zimekuwa zikinyesha tokea juzi Jumanne Desemba 20, 2011, Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi Amina. Pia tunatoa pole kwa walioumia na kupoteza mali zao katika mafuriko haya. 

Watanzania, waathirika wa mafuriko wanahitaji michango yetu kwa hali na mali kwa chochote kile ulichojaaliwa, kwa sasa waathirika hao wamejikusanyika shule mbalimbali za msingi na sekondari, vituo vya kupeleka misaada hiyo kwa sasa ambavyo vinajulika ni :-
- Azania Sekondari
- Magomeni
- Msimbazi
- Mchikichini
- Kibasila
- Magomeni
- Uhuru mchanganyiko
- Hananasifu
- Rutihinda
 inahuzunishaje!

                                         siyo jangwani peke yake hapa ni kitunda

                                    barabara nyingi zilikuwa zimefungwa

No comments: