Pages

Ads 468x60px

Wednesday 21 December 2011

KONA YA MAPISHI

Kuku Wa Tanduuri

 VIPIMO

 Kuku                                                      5 pounds  (vipande 20 – 25)
Ukwaju                                        ½  pakti ( kwa kikombe kimoja cha maji)
Vitungu thaumu                                              1 kijiko kikubwa cha kulia
Tangawizi                                                        1 kijiko kikubwa cha kulia
Uzile (binzari nyembamba ya unga)              1 kijiko cha chai
Pilipili manga                                                   1 kijiko cha chai
                                                                        (unaweza   kuongeza ukipenda) 
Chumvi                                                            kiasi 
Tandoori masala                                           1 kikubwa cha chai

NAMNA YA KUTAYARISHA .

1.   Watoe ngozi  na wasafishe vizuri halafu wachuje.
2.   Loweka ukwaju na maji kiasi cha kikombe kimoja  uvuruge mpake upate urojo mzito, uchuje kama tui la nazi kutoa kokwa kisha umimine urojo kwenye kuku.  
3.  Tia vitungu saumu na tangawizi vilivyosagwa changanya vizuri na kuku na urojo wa ukwaju.
4.  Kisha tia pilipili manga na uzile na chumvi.(chumvi unaweza kuongeza kidogo kwani wakati wa kuchoma kuku watachuja maji hivyo weka ya kutosha).
5. Tia tandoori masala  changanya
6. Changanya vizuri na waache wakolee kama nusu saa(dakika 30 hivi)

NAMNA YA KUWACHOMA.
  
1.       Kama una oven ya kawadia basi wapange kuku kwenye nyavu ya juu ya oven na weka treya tupu kwenye nyavu ya pili.
2.      Kwenye kifungo cha selector, weka grill na kwenye kifungo cha temperature weka grill vile vile na watachomeka kwa moto wa juu.
3.      Waache wachomeke kama dakika 25 hadi 30 hivi, huku watakuwa wanachuja maji na yatakuwa yanadongoka kwenye treya tupu.
4.      Wakishakauka na kubadilika rangi vizuri, ondoa treya ya maji yaliyotoka kwenye kuku.
5.       Kisha badilisha kifungo cha selector weka bake na kwenye kifungo cha temperature weka 350º weka kama dakika 10 hadi 15 watachomeka kwa moto wa chini.
6.      Kubadilisha vifungo na moto wa kuchomea kunasaidia kuku kuchomeka pande zote mbili bila ya kugeuza geuza.
7.       Wakishakauka vizuri watoe, panga kwenye sahani na saladi au pilipili ya kusaga, au chatine. Tayari kwa kuliwa.

No comments: