Wali Wa Kichina Na Mayai
Vipimo
Mchele (Basmati) 3 vikombe
Mbogamboga za barafu
(karot, njegere, spring beans na mahindi) 1 kikombe
Kuku Kidari 1 LB (ratili)
Mayai 2 mayai
Vitunguu (vikubwa) 2 au 3 vidogo
Pili pili manga 1 kijiko cha chai
Paprika 1 kijiko cha chai
Chumvi Kiasi
Mafuta 1/3 kikombe cha chai
Thomu 1 kijiko cha supu
Tangawizi 1 kijiko cha chai
Kidonge cha supu 1
Soy sauce 2 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku
- Kata kidari cha kuku vipande vidogo vidogo vya kiasi.
- Tia mafuta kidogo katika wok (karai ya kichina) kisha mtie kuku, thomu, tangawizi, soy sauce, pilipilimanga, paprika chumvi.
- Tia mboga za barafu, kidonge cha supu, kaanga kuku na mboga viwive yitu vyote na mchanganyiko ukauke.
Namna Ya Kutayarisha Na kupika Wali
- Roweka mchele wa basmati kwa muda wa saa au zaidi.
- Halafu chemsha mchele pamoja na chumvi, uache uchemke hadi ukaribie kuwiva. Chuja maji.
- Katika sufuria, tia mafuta kidogo tu, kisha tia mayai mawili ukaange haraka haraka. (crumbled egg)
- changanya mchanganyiko wa kuku na mboga. Kisha tia wali changanye vizuri.
- Rudisha katika moto, funika upikike kidogo hadi uive.
No comments:
Post a Comment