Viazi Vya Kuoka
Vipimo
Viazi 8-10
kitunguu 1
pilipili mboga(kijani/jekundu) 1
pilipili manga kiasi
chumvi kiasi
siagi 2 vijiko vya chakula
Namna Yakutayarisha
1. Vioshe
viazi vizuri kisha kata kila kiazi vipande vinne na maganda yake kisha
vichemshe kidogo tu na chumvi mwaga maji tia kwenye treya ya kuchomea.
2. Kwenye kikaangio kaanga vitunguu na mapilipili mboga kiasi halafu mwagia kwenye treya ya viazi.
3. Changanya na chumvi na pilipili manga kisha tia kwenye oveni kwa moto wa 350°F kwa dakika 15-20 vitoe na tayari kwa kuliwa.
No comments:
Post a Comment