Saladi Ya Mtindi, Karoti na Tango
Vipimo
Karoti 3
Tango 1 kubwa
*Kitunguu chekundu au cha majani (spring onion) 1 kiasi
Mtindi (Yoghurt) 1 ½ gilasi
Maji ¼ kikombe
Chumvi kiasi
Pilipili manga au nyekundu ya unga ½ kijiko cha chai
Pilipili mbichi 1
Namna Ya Kutayarisha
- Chuna (grate) karoti weka kando
- Katakata tango na kitunguu vipande vidogo vidogo .
- Katakata pilipili mbichi au isage.
- Tia mtindi katika bakuli la saladi, ongeza maji kidogo tu kiasi uchanganye vizuri.
- Tia vitu vyote uchanganye vizuri ikiwa tayari.
Kidokezo:
Ikiwa utatumia kitunguu cha majani tumia kiasi cha misongo (bunch) 3.
No comments:
Post a Comment