Pweza Wa Kukaanga
Vipimo
Pweza 1 Kilo
Mafuta ½ kikombe
Chumvi 1 kijiko cha chai
Tangawizi mbichi iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Thomu iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Masala ukipenda 1 kijiko cha supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha pweza kisha mkatekate
- Mtie viungo vyote ulotayarisha na chumvi
- Muache nusu saaa akolee viungo
- Mtie ndani ya sufuria bila maji mfunike kisha weka jikoni, atatumbuka maji mwenyewe kwa moto wa kiasi paka awe rangi ya damu yam zee (maroon)
- Akishawiva kwa rangi hiyo basi sasa mwaga maji yote,chukua pweza pekee weka kwenye bakuli au sahani
- Weka karai au kikaango (frying pan) motoni tia mafuta acha kwa muda wa dakika tano hivi mafuta yapate moto.
- Mimina pweza kwenye karai aacha wakaangike paka wabadilike ukiwageuza geuza kila baada ya muda wa dakika kumi hivi. Pweza tayari kwa kuliwa kwa ugali au muhogo
Kidokezo:
Unaweza kumwagia masala kiasi baada ya kukaanga kama picha inavyo onyesha.
No comments:
Post a Comment