Samaki Na Rojo La Koliflawa
Vipimo
Samaki nguru (king fish) 6 Vipande au wazima
Thomu na tangawizi ya kusaga 1 kijiko cha supu
Chumvi kiasi
Pilipili nyekundu ya unga 2 vijiko vya chai
Bizari ya samaki (au yoyote upendayo) 1 kijiko cha chai
Ndimu 3 vijiko vya supu
Mafuta ya kukaangia
Koliflawa ½
Viazi 4
Vitunguu 3
Nyanya 4
Nyanya kopo 2 vijiko vya supu
Pilipili mbichi 3
Pipilipili manga 1 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Mafuta ya Kupikia Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika samaki:
- Changanya vitu vyote katika bakuli ufanye lahamu (paste) ya kupakia samaki.
- Paka samaki lahamu kisha mroweke kwa muda mdogo tu.
- Kaanga samaki kisha weka kando.
Rojo La Koliflawa:
1. Chambua koliflawa kisha panga katika treya ya kupikia ndani ya oveni.
2. Nyunyizia chumvi na pilipili ya unga kidogo tu, kisha pika kwa moto wa kiasi 350° F kwa muda mdogo tu kiasi yaive nusu yake tu. Epua na weka kando.
3. Menya na katakata viazi vya mviringo ukaange katika mafuta, toa weka kando.
4. Katika karai nyingine, tia mafuta vijiko viwili vya supu, kaanga vitunguu vilokatwakatwa hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (brown) isiyokoza.
5. Katakata nyanya, pilipilii mbichi, kaanga pamoja na vitunguu.
6. Tia nyanya kopo, chumvi, pilipili manga, changanya vizuri.
7. Tia maji kiasi robo kikombe uchanganye iwe sosi.
8. Tia koliflawa na viazi changanya kidogo tu.
9. Panga samaki katika chombo au sahani ya kupakulia.
10. Mwagia sosi juu yake ikiwa tayari kuliwa kwa wali au mkate.
Kidokezo:
Samaki ukipenda mchome (bake/grill) katike oveni . Ikiwa utamchoma (bake) unaweza kumchoma pamoja na koliflawa.
No comments:
Post a Comment