Chang’a ametoa
maagizo hayo katika ziara yake yakujitambulisha katika wilaya hiyo ambapo
anatembelea kata zote 17 za wilaya yaKalambo iliyozaliwa baada ya ya wilaya mama
ya Sumbawanga kugawanywa.
Katika maagizo yake,
Chang’a pia amewataka viongozi haowanafunzi ambao hawakuripo mpaka sasa,
wanaripoti shuleni mara baada ya shuleza sekondari kufunguliwa mapema mwezi
Julai, ambapo katika kata ya Kasangailiyopo mwambao wa ziwa Tanganyikawanafunzi
40 hawakuripoti kidato cha kwanza kati ya 80 waliochaguliwa ikiwa nisawa na
asilimia 50, huku wengine 56 wakishindwa kuripoti katika Kata ya
Mkowe.
“Katika hili la elimu
sitaki mchezo kabisa…ni bora tuonanewabaya kwa sababu kumkosesha mtoto elimu ni
sawa na kumuua” alisema Mkuu huyo wa wilaya ambapo aliwatakawatendaji wa Kata
na Vijiji kushirikiana na walimu wakuu wa shule za sekondarikumaliza tatizo
hilomara moja.
Mkuu huyo wa wilaya
ameanza ziara hiyo siku mbili tu baadaya kuripoti katika kituo chake cha kazi,
ambapo amekuwa akiwaeleza wakazi wawilaya hiyo utajiri wa fursa zilizopo na
kuwataka wazitumie kwa ipasavyo ilizisaidie kuleta maendeleo ya haraka ndani na
nje wilaya hiyo.
Amezitaja baadhi ya
fursa za kiuchumi kuwa ni pamoja naKilimo cha mazao mbalimbali kama vile
mahindi, alizeti,maharage, mihogo, napamoja na ufugaji wa nyuki kwa njia ya
kisasa kwa kuweka mizinga ya nyukikuzunguka mashamba ya alizeti ili wasadie
kuchavusha alizeti na pia kupataasali nyeupe ambayo bei yake ni kubwa katika
soko la dunia.
“Asali nyeupe ni
utajiri mkubwa kwa sasa, kuna makampuniyanayoinunua kwa bei ya shilingi 150,000
kwa lita moja tu…na mimi ninamawasiliano na makampuni haya kwa hiyo nawapa hii
changamoto, kila mkulimaatakayelima alizeti aweke na mizinga ya nyuki kuzunguka
shamba lake”alisisitiza.
Kwa upande wao,
wakazi wa wilaya hiyo wamemwelezea Mkuu wawilaya yao kuwa tumaini jipya katika
kuletamaendeleo ya wilaya yaona kwamba watashirikiana naye katika kuchapa kazi,
huku wakiishukuru Serikalikukubali ombi la kuwapatia wilaya
hiyo.
No comments:
Post a Comment