Pages

Ads 468x60px

Friday, 25 May 2012

Tuesday, 22 May 2012

KONA YA MAPISHI

Pweza Wa Kukaanga

Vipimo


Pweza                                                                   1 Kilo

Mafuta                                                                   ½ kikombe

Chumvi                                                                  1 kijiko cha chai

Tangawizi mbichi iliyosagwa                                    1 kijiko cha chai

Thomu iliyosagwa                                                  1 kijiko cha chai

Masala ukipenda                                                    1 kijiko cha supu



Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Osha pweza kisha mkatekate  
  2. Mtie viungo vyote ulotayarisha  na   chumvi
  3. Muache nusu saaa akolee viungo
  4. Mtie ndani ya sufuria bila maji mfunike kisha weka jikoni, atatumbuka maji mwenyewe kwa moto wa kiasi paka awe rangi ya damu yam zee (maroon)
  5. Akishawiva kwa rangi hiyo basi sasa mwaga maji yote,chukua pweza pekee weka kwenye bakuli au sahani
  6. Weka karai au kikaango (frying pan) motoni tia mafuta  acha kwa muda wa dakika tano hivi mafuta  yapate moto.
  7. Mimina pweza kwenye karai aacha wakaangike paka wabadilike ukiwageuza geuza kila baada ya muda wa dakika kumi hivi.  Pweza tayari kwa kuliwa   kwa ugali au muhogo

Kidokezo: 

Unaweza kumwagia masala kiasi baada ya kukaanga kama picha inavyo onyesha.

Sunday, 13 May 2012

ZAWADI MUHIMU KWA CKU YA LEO KWA MAMAZ......

                                          Cathy akiwa na zawadi aliomuandalia mamae
                                                            Diana akijilamba jikekii
                                                                     Diana na wanae

IT'S ALL ABOUT MATHOER'S DAY!!!............(UPENDO WA MAMA NI WA HALI YA JUU)

                                                          Hawa na bintiye Brianna
                                                   Susan na mwanae Nicole

                                                        Sarah na bintiye Raqsah
                                           Davina a.k.a 'mama jr' na bintiye Emmy
                               Lulu 'mamaa wa unique pearl collection' na bintiye Sandra
                                                  Lulu na fest bonn wake Sarah

                                                     Margareth na bintiye Asha
                                              Diana na wanae 'Cathy na chriss'
                                                               Aisha na bintiye Asma
                                                    Mariam na mwanae Nayla

                                           Khadija na mwanae Malcom
                             Swaumu a.k.a 'mama Kayla' na mwanae Jameel
                                                    Mii na my binti Faiza Shahina

Tuesday, 8 May 2012

ATAEWAKILISHA NIGERIA KTK ''LITTLE MISS WORLD''.................FREDA - ANN EKO

                                                     akiwa na umri wa miaka 11


Monday, 7 May 2012

POWWZZ


ANAHITAJI MSAADA (AKIMBIWA NA MUME BAADA YA WATOTO KUVIMBA VICHWA)


undefined
Sophia Rashid.

“HAYA ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu na si kazi ya binadamu, nasikitika kwa sababu mume wangu amenitelekeza baada ya kuona watoto wamevimba kichwa,” hayo ni maneno yaliyotamkwa na Sophia Rashid , 22, mkazi wa Chanika nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambaye anauguza wanaye wawili wanaosumbuliwa na uvimbe wa kichwa.

Mama huyo alisema watoto wake hao aliwazaa wakiwa na matatizo ya kuvimba vichwa kutokana na kujaa maji, hali ambayo inamfanya akose raha.

“Kwangu sasa imekuwa ni matatizo makubwa mwanangu Omari mwenye miaka minne na Maulid mwenye miezi kumi wanasumbuliwa na ugonjwa mmoja ambao umesababisha baba yao kuwakimbia,” alisema mama huyo akiwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi)…
Aliongeza kuwa, tangu alipofika hospitalini hapo wiki mbili zilizopita, amekuwa akipata msaada kutoka kwa maofisa wa ustawi wa jamii wa Moi lakini ndugu zake hawafiki kabisa kumjulia hali.
Daktari mmoja hospitalini hapo aliyezungumza kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini alisema kuwa, hali hiyo huwapata watoto kutokana na kuwa na upungufu wa madini ya pholic acid na mjamzito kukosa lishe bora wakati wa ujauzito.
MSAADA
Kutokana na matatizo hayo mama huyo anaomba kusaidiwa na mtu yeyote aliyeguswa na masaibu yake kifedha, chakula, mavazi, dawa pamoja na kipimo cha TC Scan ambacho alidai kuwa kipo katika Hospitali ya Regency ya jijini Dar es Salaam na gharama yake ni shilingi 258,000 kwa mtoto mmoja.
Atakayependa kumsaidia mama huyo atumie simu namba 0716755384 au afike Hospitali ya Muhimbili, Moi kwenye wodi A.


 habari na GLOBAL PUBLISHERS

Saturday, 5 May 2012

EMMY'S 2ND BIRTHDAY

                                                                 jikeeeekii
                                                  Birthday girl ''EMMY''
                                Davina na wanae Juniour na Emmy

Tuesday, 1 May 2012

KONA YA MAPISHI


       Saladi Ya Mtindi, Karoti na Tango


  undefined

Vipimo


Karoti                                                                              3

Tango                                                                             1 kubwa

*Kitunguu chekundu  au cha majani (spring onion)            1 kiasi

Mtindi (Yoghurt)                                                              1 ½ gilasi

Maji                                                                                ¼ kikombe

Chumvi                                                                           kiasi

Pilipili manga au nyekundu ya unga                                   ½ kijiko cha chai

Pilipili mbichi                                                                    1


Namna Ya Kutayarisha


  1. Chuna (grate) karoti weka kando

  1. Katakata tango na kitunguu vipande vidogo vidogo  .

  1. Katakata pilipili mbichi au isage.

  1. Tia mtindi katika bakuli la saladi, ongeza maji kidogo tu kiasi  uchanganye vizuri.

  1. Tia vitu vyote uchanganye vizuri ikiwa tayari.


Kidokezo:

Ikiwa utatumia kitunguu cha majani  tumia kiasi cha misongo (bunch) 3.