Pages

Ads 468x60px

Wednesday, 11 July 2012

MKUU WA WILAYA MPYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA APOKELEWA KWA SHANGWE

MKUU wa wilaya mpya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa Moshi MussaChang’a amewaagiza viongozi wa kata za wilaya hiyo kuhakikisha wanawachukuliahatua kali za kisheria wazazi wa wanafunzi ambao walifaulu na kuchaguliwa kuingiakidato cha kwanza mwaka huu lakini hawajaripoti shuleni mpaka sasa ambapomuhula wa kwanza masomo umemalizika.

undefined
Chang’a ametoa maagizo hayo katika ziara yake yakujitambulisha katika wilaya hiyo ambapo anatembelea kata zote 17 za wilaya yaKalambo iliyozaliwa baada ya ya wilaya mama ya Sumbawanga kugawanywa.

Katika maagizo yake, Chang’a pia amewataka viongozi haowanafunzi ambao hawakuripo mpaka sasa, wanaripoti shuleni mara baada ya shuleza sekondari kufunguliwa mapema mwezi Julai, ambapo katika kata ya Kasangailiyopo mwambao wa ziwa Tanganyikawanafunzi 40 hawakuripoti kidato cha kwanza kati ya 80 waliochaguliwa ikiwa nisawa na asilimia 50, huku wengine 56 wakishindwa kuripoti katika Kata ya Mkowe.

“Katika hili la elimu sitaki mchezo kabisa…ni bora tuonanewabaya kwa sababu kumkosesha mtoto elimu ni sawa na kumuua” alisema Mkuu huyo wa wilaya ambapo aliwatakawatendaji wa Kata na Vijiji kushirikiana na walimu wakuu wa shule za sekondarikumaliza tatizo hilomara moja.

Mkuu huyo wa wilaya ameanza ziara hiyo siku mbili tu baadaya kuripoti katika kituo chake cha kazi, ambapo amekuwa akiwaeleza wakazi wawilaya hiyo utajiri wa fursa zilizopo na kuwataka wazitumie kwa ipasavyo ilizisaidie kuleta maendeleo ya haraka ndani na nje wilaya hiyo.

Amezitaja baadhi ya fursa za kiuchumi kuwa ni pamoja naKilimo cha mazao mbalimbali kama vile mahindi, alizeti,maharage, mihogo, napamoja na ufugaji wa nyuki kwa njia ya kisasa kwa kuweka mizinga ya nyukikuzunguka mashamba ya alizeti ili wasadie kuchavusha alizeti na pia kupataasali nyeupe ambayo bei yake ni kubwa katika soko la dunia.

“Asali nyeupe ni utajiri mkubwa kwa sasa, kuna makampuniyanayoinunua kwa bei ya shilingi 150,000 kwa lita moja tu…na mimi ninamawasiliano na makampuni haya kwa hiyo nawapa hii changamoto, kila mkulimaatakayelima alizeti aweke na mizinga ya nyuki kuzunguka shamba lake”alisisitiza.

Kwa upande wao, wakazi wa wilaya hiyo wamemwelezea Mkuu wawilaya yao kuwa tumaini jipya katika kuletamaendeleo ya wilaya yaona kwamba watashirikiana naye katika kuchapa kazi, huku wakiishukuru Serikalikukubali ombi la kuwapatia wilaya hiyo.

No comments: