Vipimo
Viazi (mbatata) ¼ kilo (kiasi viazi 5) au vitano
Limau au ndimu au siki ½ kikombe
Vitunguu nyasi (spring onions) 4-5 miche
Mafuta ya zaituni (oliven oil) ½ kikombe
Chumvi Kijiko cha chai kimoja na nusu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Chemsha viazi na maganda yake hadi viive bila ya kuvurujika
- Viache vipowe kisha chambua viazi ukatekate slesi au vidogodogo, mimina ndani ya bakuli kubwa.
- Katakata vitunguu tia kwenye viazi, tia chumvi na mafuta ya zaituni, limau kisha vichanganye uzuri.
- Onja chumvi na limau ukiona yametokeza ladha basi saladi tayari kwa kuliwa.
Kidokezo;
- Hii ni saladi huliwa sana wakati wa majira ya joto (summer). Waweza kula saladi hii kwa nyama ya kuchoma au samaki.
No comments:
Post a Comment