OKRA/BAMIA ZA KUKAANGA
Vipimo:
Bamia
Kitunguu 1
Kitunguu thomu 3 chembe
Methi/Uwatu/fenugreek ilosagwa ½ kijiko cha chai
Pilipili manga ½ kijiko cha chai
Pilipili mbichi 1
Chumvi kiasi
Mafuta 3 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha okra/bamia kata vikonyo, kisha zikate vipande kwa urefu.
- Katakata kitunguu maji, kitunguu thomu, pilipili mbichi weka kando.
- Weka mafuta katika karai kisha kaanga kitunguu hadi kianze kugeuka rangi kuwa hudhurungi (golden brown) kisha tia kitunguu thomu kaanga kidogo tu.
- Tia bamia, pilipili mbichi, methi, pilipili mbichi, chumvi endelea kukaanga kwa moto mdogo mdogo hadi bamia ziwive na ziwe tayari.