Pages

Ads 468x60px

Monday, 15 August 2011

kona ya mapishi

kachori

mahitaji
viazi mbatata 2lb

thomu na tangawiz kijiko kimoja cha chakula

ndim moja

mafuta ya kupikia

unga wa ngano au wa dengu kiasi

namna ya kutayarisha


1.chemsha viazi mpaka viive kisha vitoe maganda na uviweke ndani  ya bakuli
2.viponde ponde mpaka viwe laini

3.saga thomu na tangawizi kisha changanya na viaz


4.weka chumvi ndimu na pilipili ya unga kisha uonje unaweza ongeza viungo hivi kadri ya mapenzi yako

5.tengeneza madonge ya duara uyapange katika tray

6.vuruga unga wa dengu au wa ngano kwa maji uwe mwepesi kidogo

7.weka mafuta ya kupikia ndani ya karai na uliweke kwenye moto

8.chovya madonge kwenye unga na uyatose kwenye mafuta ya moto(uchomaji wake ni kama bajia)

9.wacha kachori zibadilike rangi na kuwa za njano na uzitoe kwenye mafuta 

10.weka kachori kwenye sahani zipoe na tayari kuliwa

mapishi haya yameletwa na mama Abra

No comments: