SAMBUSA ZA VIAZI

Vipimo
Viazi                                                                          4
Vitunguu nyasi vilokatwakatwa                                    3 miche
Kitunguu maji kilokatwakatwa                                     1
Chumvi                                                                     1 kijiko cha chai
Bizari ya pilau nzima ( jeera)                                      1 kijiko cha chai
Mafuta                                                                       Nusu kilo
Manda za tayari                                                         10 - 20                                
Yai                                                                            1 au 2
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Menya viazi, vioshe vikate slesi kisha  vikatekate vipande vidogo vidogo.

- Chemsha maji kidogo ukiwa umeyatia chumvi , kisha vimimine viazi ndani ya maji yawache paka uwone tena yachemka kwa mara ya pili acha kwa dakika 10 - 15, kisha ondoa jikoni.
- Mimina katika chujio uchuje maji .
- Roweka bizari kwenye maji kwa muda wa dakika 20 hivi.
- Chukua bakuli kubwa lenye nafasi mimina viazi, vtunguu nyasi na maji,   chumvi, mafuta vijiko 2 – 3 vya supu, na bizari. Changanya vizuri.
- Tandaza manda mezani au kwenye kibao fanya mkunjo wa sambusa kisha paka yai kwa brashi, kunja upate pembe moja . Tazama picha.

- Jaza viazi sehemu ulokunja kisha funga sambusa.
 
     
- Tia mafuta katika karai, yakipata moto, tia sambusa ziikaange hadi zigeuke rangi ya dhahabu.  
- Zitoe na zichuje mafuta tayari kuliwa kwa Sosi Ya Ukwaju au Chatine Ya Mtindi
 

 



















 
 
 
 
 
 
 
 
