Pages

Ads 468x60px

Sunday, 30 September 2012

BARABARA ZA LAMI ZINAZOENDELEA KUJENGWA MKOANI RUKWA TUMAINI JIPYA KWA WAKAZI WA MKOA HUO

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi waliokutwa na Kamera yetu wakifurahia ujio wa barabara za lami zinazoendelea kujengwa Mkoani Rukwa zikiunganisha Mkoa huo na Mikoa ya Mbeya na Katavi.
Baadhi ya wakandarasi wanaojenga barabara ya Laela-Sumbawanga wakiwa kazini. Kwa sasa kasi ya ujenzi wa barabara za Tunduma-Ikana, Ikana-Laela, Laela-Sumbawanga, na Sumbawanga-Kasanga imeongezeka ikilinganishwa na hapo awali.


Picha na habari shukraan ofisi ya mkuu wa mkoa Rukwa

Sunday, 23 September 2012

SHAQEEL'Z 3RD BIRTHDAY..........


                                                                  La 'birthday boy'
                                                 Mamie akimsaidia kukata mikekiii

                                                               Watoto wakijiachia





FILAMU MPYA KITAANI


Tuesday, 18 September 2012

TOTO KONA

                                                   Sameera a.k.a 'Minglee'

HANDBAGS TOKA UK.......................MPIGIE 'LEYLA 0712020777 '

                                                                     Tsh 62,000




                                                                         Tsh 62,000

                                                                       Tsh 72,000


                                                                        Tsh 62,000

Saturday, 8 September 2012

POWWZZZ


KONA YA MAPISHI

SALADI YA MAHINDI


Vipimo
Majani ya saladi (lettuce) ½ msongo
Kabeji ya Zambarau ¼
Mahindi 1 kikombe
Tango 1
Kitunguu majani (spring onion) 3
Nyanya 2

Salsali (salad dressing)
Thomu iliyosagwa 2 chembe
Chumvi kiasi
Ndimu au siki 2 jiko vya supu
Mafuta ya zaytuuni ¼ kikombe
Pilipili ya unga nyekundu ½ kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha

  1. Katakata majani ya saladi, kabeji, weka katika bakuli.
  2. Menya tango, katakata tia pamoja.
  3. Chemsha mahindi au tumia ya tayari ya kopo, mwaga maji.
  4. Katakata kitunguu majani, nyanya.
  5. Changanya vitu vyote pamoja.
  6. Tayarisha Salsali yake kwa kuchanganya vitu vyote, weka kando hadi wakati wa kula umwagie juu yake na uchanganye vizuri. 

HONGERA SAANA LIL' KAZIN...............NEGIYE AMRI


Tuesday, 4 September 2012


DRESSED BY ..............''UNIQUE PEARL COLLECTION''

                                                                     top,skirt & handbag

Monday, 3 September 2012

CCM Uingereza Yasuka Upya Safu Ya Uongozi




Chama Cha Mapinduzi nchini Uingereza jana kilisuka upya safu yake ya uongozi kwa kuchagua viongozi wapya na kuongeza nafasi mpya za manaibu katika Sekretarieti ili kuboresha utendaji. Aidha kikao kilikaa kwa utaratibu maalum na kuridhia kwa pamoja kuongeza nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Tawi kutoka Zanzibar.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Tawi ilijazwa na Ndugu Sukwa Said Sukwa aliyepita bila kupingwa ili kuleta uwiano wa kitaifa.
Safu mpya za uongozi wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi UK na miji watokayo kwenye mabano ni kama ifuatavyo:

1.0 Katibu wa CCM wa Tawi ni Bi. Mariam Mungula. (East London)
1.1.Naibu Katibu wa CCM Tawi ni Ndugu Albert Ntemi. (Luton)

2.0 Katibu wa Siasa na Uenezi Tawi ni Ndugu Leybab Mdegela (Northampton)
2.1 Naibu Katibu wa Siasa na uenezi Tawi ni Ndugu Abraham Sangiwa (Luton)

3.0 Katibu wa Uchumi na Fedha wa Tawi ni Ndugu John Lyimo (Manchester)
3.1 Naibu Katibu wa Uchumi na Fedha ni Ndugu Mohamed Upete (Reading)
4.Kikao hicho vilevile kilimteua Ndugu Haruna Mbeyu maarufu kama “Meya wa London” kuchukua wadhifa wa kuwa “Mshauri Maalum” au “Special Advisor” wa Tawi La Uingereza kutokana na mchango wake mkubwa kwa Watanzania UK.
Kikao kiliridhia pingamizi lililowekwa na wengi wa wajumbe kwa Ndugu Moses Katega kutetea nafasi yake ya Katibu wa Siasa na Uenezi kwa kuzingitia sifa, maadili na miiko ya uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi. 
Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi itaendelea kuwa na Viongozi wa Tawi na Wenyeviti wa mashina. Aidha Kamati ya Usalama na Maadili sasa itakuwa na wajumbe wafuatao:
1.Lilian Barongo - Mwenyekiti.
2.Mashamba Mashaka 
3.Kapinga Kangoma 
4.Frank Mukiza 
5.Victor Mgoya 
6. Joseph Gobbos
Kabla ya uchaguzi ambao uliendeshwa kwa demokrasia ya hali ya juu, Mwenyekiti wa Tawi Ndugu Maina Owino aliwaasa wajumbe kuzingatia haki na wajibu wa uwanachama na sifa na miiko ya uongozi kama ilivyoainishwa katika miongozo na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi.
Kikao kilipokea taarifa muhimu ya Kamati Maalum, kilibariki marekebisho ya mwisho ya Website ya kisasa ya CCM UK na kilipitisha mipango mipya ya kuendeleza Chama kwa manufaa ya Watanzania na Wanadiaspora.

Mariam Mungula 
Katibu wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi, Uingereza 
CHAMA CHA MAPINDUZI -UK. 
Imetolewa na Idara ya Siasa na Uenezi, Tawi la CCM ,Uingereza.

Saturday, 1 September 2012

MPENDE MWANAO




                                                           350,000/=TSH
                                          Jaguar for your child 550,000/= TSH only


                                                                390,000 TSH
                                                                   315,000 TSH