Pages

Ads 468x60px

Saturday, 8 September 2012

KONA YA MAPISHI

SALADI YA MAHINDI


Vipimo
Majani ya saladi (lettuce) ½ msongo
Kabeji ya Zambarau ¼
Mahindi 1 kikombe
Tango 1
Kitunguu majani (spring onion) 3
Nyanya 2

Salsali (salad dressing)
Thomu iliyosagwa 2 chembe
Chumvi kiasi
Ndimu au siki 2 jiko vya supu
Mafuta ya zaytuuni ¼ kikombe
Pilipili ya unga nyekundu ½ kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha

  1. Katakata majani ya saladi, kabeji, weka katika bakuli.
  2. Menya tango, katakata tia pamoja.
  3. Chemsha mahindi au tumia ya tayari ya kopo, mwaga maji.
  4. Katakata kitunguu majani, nyanya.
  5. Changanya vitu vyote pamoja.
  6. Tayarisha Salsali yake kwa kuchanganya vitu vyote, weka kando hadi wakati wa kula umwagie juu yake na uchanganye vizuri. 

No comments: