KILA LA KHERI TAIFA STARS
CAPTAIN JUMA KASEJA NA KIKOSI CHAKO CHA KAZI, NAPENDA KUWATAKIA KILA LA KHERI KESHO MTAKAPOTINGA HAPO VIWANJA VYA GRAND STADE MJI WA MARRAKECH KUPAMBANA NA MOROCCO.
NINA IMANI YA KUWA WATANZANIA WOTE TUKO NYUMA YENU, TUNAWAAMINI NA TUNATHAMINI UZALENDO WENU. TUNA IMANI YA KUWA MTATUMIA WEMBE ULEULE MLIOWANYOLEA HAWA WAMOROCCO UWANJA WA TAIFA NA KUWABWAGA 3-1, KWA MAKALI YALE, AMA ZAIDI KWA NIA MOJA TUU YA KUFIKA BRAZIL 2014 ……
PAMOJA NA SALAMU NAPENDA KUWATAARIFU KUWA WANA DIASPORA WA LONDON TUMEJIPANGA VIZURI ILI KUWA NYUMA YENU KATIKA SAFARI YOTE . KIKOSI KABAMBE CHA WASHANGILIAJI, KIMEONDOKA LONDON JIONI HII KUJA MARRAKECH ILI KUWAUNGA MKONO.
KIKOSI HICHO, KIKIONGOZWA NA “MEYA WA JIJI” SIR.HARUNA MBEYU, KITAKUWA PALE “GRAND STADE” NA MAVUVUZELA YA HATAREEEE TAYARI KWA MPAMBANO HUO.
TUKO BEGA KWA BEGA NA NYINYI MPAKA 2014 NDANI YA “ESTADIO DO MARACANA”, RIO DE JANEIRO……
NAWATAKIA USHINDI MKUBWA NA MCHEZO MWEMA “FAIR PLAY”.
MWENYEZI MUNGU IBARIKI TAIFA STARS.
MWENYEZI MUNGU IBARIKI TANZANIA.
TAIFA STARS OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE……………!!
Mariam Mungula -MwanaDiaspora
#TeamTaifaStarsUK.
No comments:
Post a Comment