Shurba Ya Nyama Mbuzi
VIPIMO
Nyama ya mbuzi ya mafupa au ya ng'ombe Kilo moja
Mafuta 2 vijiko vya supu
Vitunguu maji (vikate vidogo vidogo) 2
Nyanya (kata ndogo ndogo) 1
Thomu na tangawizi iliyosagwa 2 vijiko vya supu
Bizari ya pilau ya unga (Jeera) 1 kijijo cha chai
Gilgilani ya unga (Dania) ½ kijiko cha chai
Pilipili manga ya unga 1 kijiko cha chai
Mdalasini wa unga ¼ kijiko cha chai
Kotmiri (iliyokatwa ndogo ndogo) kiasi
Nanaa (iliyokatwa ndogo ndogo) kiasi
Chumvi kiasi
Siki 3 vijiko vya supu
Shayiri (Oats) au * 2 vikombe
* ikiwa shayiri nzima nzima, basi roweka kwa muda wa masaa na uchemshe mpaka ziive.
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Chemsha nyama na chumvi kwa maji kiasi mpaka iwive
2. Katika sufuria nyengine, weka mafuta na kaanga vitunguu kidogo tu vilainike, usiviwache kugeuka rangi.
3. Weka bizari zote, pili pili manga, chumvi.
4. Tia thomu na tangawizi.
5. Tia nyanya na bila ya kuzikaanga sana tia nyama na supu yake.
6. Tia kotmiri, nanaa.
7. Pembeni changanya shayiri (oats) na maji koroga kisha tia katika supu ya shurba.
8. Iwache ichemke kidogo tu ngano ziwive.
9. Tia siki na tayari kuliwa.
No comments:
Post a Comment