Pages

Ads 468x60px

Thursday, 12 January 2012

powzz


KONA YA MAPISHI

CHAPATI ZA KUKU

VIPIMO
 Kuku wa kusaga 1lb

Nyanya 1 ndogo

Thomu 1½ kijiko cha chai

Tangawizi 1 kijiko cha chai

Pilipili manga 1 kijiko cha chai

Bizari unataka ½ kijiko cha chai

Kidonge cha supu 1

Pilipili mbichi 1 au 2

Chumvi kiasi

Vitunguu vya majani kiasi

Vitunguu 2

Mayai 6

Manda za tayari (spring rolls) 12

NAMNA YA KUTAYARISHA
 1. Saga nyanya, thomu, tangawizi na pilipili kwenye blender

2. Tia kima, vitu ulivyosaga, pilipili manga,kidonge cha supu, chumvi na bizari.

3. Weka motoni huku ukichanganya mpaka ikauke.

4. Kisha iache pembeni ipoe.

5. Kisha kata kata vitungu Kama vya sambusa na vitungu vya majani.

6. Chukuwa bakuli tia kima kama vijiko 4 au zaidi vya supu

7. Tia vitunguu vyote aina mbili kiasi na mayai mawili.

8. Chukuwa sinia ya oveni tia mafuta kama vijiko 2 au zaidi kidogo

9. Kisha panga manda 2 kwenye sinia.

10. Changanya mchanganyiko kwenye bakuli mimina juu ya manda utandaze.

11. Kisha funika manda 2 nyingine kwa juu na waweza kufanya 3 kwa pamoja.

12. Choma kwenye oveni moto wa chini ikishaiva tia mafuta geuza upande wa pili epua na itakuwa tayari kuliwa.

Tuesday, 10 January 2012

WASAIDIE WATOTO HAWA




KATIKA gazeti la Uwazi, toleo la wiki iliyopita walitoa habari za mtoto Mustafa Ally, 12, (pichani), mkazi wa Mtoni Mtongani, Wilaya ya Temeke  jijini Dar es Salaam anayewauguza wadogo zake  mapacha wenye umri wa miezi nane.
Mtoto Mustafa ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Twiga, Temeke amelazimika kuwauguza wadogo zake hao, Swaumu na Ramadhani kwa kuwa  baba yao alishafariki na mama yao yupo mahututi.
Watoto hao mapacha wanaumwa na wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu. Mama yao aliyekuwa akiwauguza aliugua ghafla na kupewa matibabu na kwa sasa yupo hoi nyumbani kwake, hivyo Mustafa kuchukua mzigo huo wa kuwauguza.
Matatizo yanayoikabili familia hiyo ni pamoja na ukosefu wa chakula, nguo za kawaida na za shule, fedha za matumizi, maziwa ya unga ya watoto na kodi ya nyumba.
Gazeti hilo kwa niaba ya familia hiyo linatoa shukrani kwa watu mbalimbali waliompatia msaada wa maziwa, sabuni, sukari, nguo na fedha, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 300,000.
Bado msaada unakaribishwa kwa watoto hawa. Aliyeguswa na kilio cha mtoto Mustafa afanye mawasiliano na Afisa Ustawi wa Jamii Muhimbili,  Erika Ishengoma kwa simu 0714 220 038 au mwandishi wetu kwa namba 0713 454 656 au afike Muhimbili wodi ya watoto, Makuti B atakutana nao ana kwa ana.



E'M E'M GET 2GETHER'Z PARTY .............@CINE CLUB

Karen & Kulwa (wakurugenzi)
                                                                          Zediy
                                                                     Zuhura
                                            Rehema....mamaa wa NOVA'S CHOICE
                                                                     Tamali
                                                                         Miriam
                                                            Karen, Kulwa & Benedicta


                                                  mishikaki ya samaki,mbuzi na ngo'mbe
                                                                makulaajii

na hili ndilo kundi la E'M E'M  Dar es salaam branch



WAKAZI WA UINGEREZA WACHANGIA WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO TANZANIA

undefined
 Louisa Frisch (Bright Future TZ), Jestina George, Haruna Mbeyu (TA London) & Chris Lukosi 'Mzee wa Kazi (Serengeti Freight)
undefined
Umi Macho, Jestina George & Louisa

undefined
  Chris, Jestina na wadau wengine wakikusanya misaada mbalimbali
undefined
Jestina akimshukuru Pr. Mattheww kwa mchango wake
undefined
Mzee wa Kazi Chris Lukosi, Louisa (Bright Future TZ), Jestina George & Pastor Matthew
 
undefined
 Haruna Mbeyu, Mzee wa Kazi (Serengeti Freight) Mohsin akimpa mkono wa shukran Naibu Balozi
 Mzee wa kazi (serengeti Freight) Chris Lukosi na Naibu Balozi
 Katibu wa CCM East London & Katibu wa TAWA UK Mariam Mungula akiwa na

undefined
 Baadhi ya viongozi wa TA London Haruna Mbeyu, Said Surur wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Balozi na dada Louisa wa Bright Future TZ
 Wazee wa kazi 'Kikazi Zaidi'

 Chris akimshukuru Iscandar kwa support yake
undefined
Viongozi wa TA London wakiwa katika picha ya pamoja na waandaji wa hrambee

undefined
Hivi ni baadhi ya vitu vilivyo patikana katika Harambee
Said Suru, Dullah Meru, Iscandar, Chris Lukosi & Jestina katika picha ya pamoja
undefined
Picha ya pamoja baada ya shughuli kuisha na baadhai ya wadau waliojitokeza kuchangia
---
Siku ya Jumamosi tarehe 7 January 2011 Serengeti freight wakishirikiana na Miss Jestina Blog, Bright Future TZ pamoja na Urban Pulse walifanya harambee maalum ya kuchangia watanzania walioathirika na mafuriko yaliotokea hivi karibuni mwishoni mwa mwaka jana  nyumbani Tanzania.

Mgeni rasmi alikuwa Naibu balozi Mh Chabaka Kilumanga.  Aidha Mh Balozi aliongea na kushukuru watanzania wote walioguswa na kujitolea kwa hali na mali ili kuweza kusaidia watanzania wenzao waliokumbwa na janga hili. Misaada bado inaendelea kupokelewa na kukusanywa mpaka mwisho wa mwezi huu wa january. Hivyo basi kwa wale wote walioshindwa kuweza kufika siku ya jumamosi kutoa michango bado  nafasi ipo. Kumbuka hili ni janga letu wote tafadhali fanya sehemu yako kwa jinsi Mungu anavyokubariki. 

KWA MAWASILIANO ZAIDI KUHUSU MISAADA WASILIANA NA
JESTINA GEORGE 07404332910
FRANK  EYEMBE 07865594576
BARAKA NYAMA 07816981577 

KAMA UNA MCHANGO UNAWEZA KUDEPOSIT KATIKA ACCOUNT IFUATAYO:
BARCLAYS BANK
JINA: TANZANIA ASSOCIATION LONDON Account Number: 23374815 
Sort Code: 20-72-89 
ANDIKA JINA LAKO NA MAFURIKO AS REFERENCE

TUNAWASHUKURU NYOTE KWA KUJALI NDUGU ZETU
Contact us for more info;
CHRIS LUKOSI 07903828119 
SIMON LOUIS (MOHSIN) 07950689243
BRIAN (BABA NJOROGE) 07795160757
HASSAN (RICHARD) 07405159255
HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477