Pages

Ads 468x60px

Monday, 7 May 2012

ANAHITAJI MSAADA (AKIMBIWA NA MUME BAADA YA WATOTO KUVIMBA VICHWA)


undefined
Sophia Rashid.

“HAYA ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu na si kazi ya binadamu, nasikitika kwa sababu mume wangu amenitelekeza baada ya kuona watoto wamevimba kichwa,” hayo ni maneno yaliyotamkwa na Sophia Rashid , 22, mkazi wa Chanika nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambaye anauguza wanaye wawili wanaosumbuliwa na uvimbe wa kichwa.

Mama huyo alisema watoto wake hao aliwazaa wakiwa na matatizo ya kuvimba vichwa kutokana na kujaa maji, hali ambayo inamfanya akose raha.

“Kwangu sasa imekuwa ni matatizo makubwa mwanangu Omari mwenye miaka minne na Maulid mwenye miezi kumi wanasumbuliwa na ugonjwa mmoja ambao umesababisha baba yao kuwakimbia,” alisema mama huyo akiwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi)…
Aliongeza kuwa, tangu alipofika hospitalini hapo wiki mbili zilizopita, amekuwa akipata msaada kutoka kwa maofisa wa ustawi wa jamii wa Moi lakini ndugu zake hawafiki kabisa kumjulia hali.
Daktari mmoja hospitalini hapo aliyezungumza kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini alisema kuwa, hali hiyo huwapata watoto kutokana na kuwa na upungufu wa madini ya pholic acid na mjamzito kukosa lishe bora wakati wa ujauzito.
MSAADA
Kutokana na matatizo hayo mama huyo anaomba kusaidiwa na mtu yeyote aliyeguswa na masaibu yake kifedha, chakula, mavazi, dawa pamoja na kipimo cha TC Scan ambacho alidai kuwa kipo katika Hospitali ya Regency ya jijini Dar es Salaam na gharama yake ni shilingi 258,000 kwa mtoto mmoja.
Atakayependa kumsaidia mama huyo atumie simu namba 0716755384 au afike Hospitali ya Muhimbili, Moi kwenye wodi A.


 habari na GLOBAL PUBLISHERS

Saturday, 5 May 2012

EMMY'S 2ND BIRTHDAY

                                                                 jikeeeekii
                                                  Birthday girl ''EMMY''
                                Davina na wanae Juniour na Emmy

Tuesday, 1 May 2012

KONA YA MAPISHI


       Saladi Ya Mtindi, Karoti na Tango


  undefined

Vipimo


Karoti                                                                              3

Tango                                                                             1 kubwa

*Kitunguu chekundu  au cha majani (spring onion)            1 kiasi

Mtindi (Yoghurt)                                                              1 ½ gilasi

Maji                                                                                ¼ kikombe

Chumvi                                                                           kiasi

Pilipili manga au nyekundu ya unga                                   ½ kijiko cha chai

Pilipili mbichi                                                                    1


Namna Ya Kutayarisha


  1. Chuna (grate) karoti weka kando

  1. Katakata tango na kitunguu vipande vidogo vidogo  .

  1. Katakata pilipili mbichi au isage.

  1. Tia mtindi katika bakuli la saladi, ongeza maji kidogo tu kiasi  uchanganye vizuri.

  1. Tia vitu vyote uchanganye vizuri ikiwa tayari.


Kidokezo:

Ikiwa utatumia kitunguu cha majani  tumia kiasi cha misongo (bunch) 3.

Sunday, 29 April 2012

@MUUNGANO DAY

                                                                      Fathiya
                                                                  Swaumu
                                                            Julieth & Swaumu


                                                     Mr & Mrs Eddie

                                                  ''nawapendaajeee''

Sunday, 22 April 2012

TASWIRA'Z..........@SHULLA'Z K.PARTY

                                            Maryam Mungula ......katibu TAWA
                                                                Salama
                                                                  Zuhura & Amina
                                                         Keyfa & Lawi
                                                               Sakina & Tatu
                                                            Zaomba
                                                             Salha & Nayla
                             Lulu mamaaaa wa 'Unique Pearl Collections'  & Dida
                                                                          Rahma
                                                                       Sakina
                                                                       Miii
                                                          'Kungwi na mwariwe'

Saturday, 21 April 2012

HOTELI ZA KITALII KTK FUKWE ZA ZIWA TANGANYIKA.....MKOA WA RUKWA

                               Hoteli ya kitalii iliyopo Kipili wilaya ya Nkas mkoani Rukwa
 Baadhi ya Hoteli zinazopatikana Mkoani Rukwa katika Wilaya ya Nkasi katika Tarafa ya Kipili. Boti zinazoonekana ni kwa ajili ya wateja watakaohitaji kwenda kucruise ndani ya Ziwa. Bado yapo maeneo maalum ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa Hoteli za Kitalii katika ukanda huu.
 Hakika mandhari haya yanavutia na hivyo ni baadhi ya vyumba katika Hoteli hiyo ya Kipili.
 Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Ally Kessy, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Nkasi wakimaliza ziara ya kukagua Fukwe za Ziwa Tanganyika huku wakielekea kwenye Hoteli ya Kipili ambayo kwa kiasi kikubwa hupata wageni wa kitalii.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (Kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana (Kushoto) wakiongea na watalii waliofikia katika Hoteli ya Kipili Wilayani Nkasi siku za hivi karibuni walipoenda kutembelea fukwe hizo.

Habari na picha akhsante OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA

Thursday, 19 April 2012

KONA YA MAPISHI

                 KUKU WA KUOKA (BAKED) NA SOSI YA UKWAJU



Vipimo
Kuku                                                                    1 mzima
Thomu na tangawizi ilosagwa                                  2 vijiko vya supu
Chumvi                                                                  Kiasi
Bizari mchanganyiko                                              2  vijiko vya supu
Pilipili mbichi kijani na nyekundu                               2-3
Ukwaju  mzito uliokamuliwa                                   ½ kikombe
Vitunguu vya kijani (spring onions)                         2 mche (stalk)
Kotmiri                                                                  1 mche (stalk)
Mafuta                                                                1 Vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Safisha kuku kisha mwache achuje maji vizuri.
  2. Katakata vitunguu, pilipili, kotmiri, weka kando.
  3. Changaya masala yote kwenye bakuli pamoja na mafuta.
  4. Mpakaze  kuku wote masala ya ukwaju nje na ndani akolee viungo. Kisha roweka kwa muda wa masaa yasipungue mawili takriban.

  1. Muweke katika treya, na bakisha sosi ulomrowekea kidogo kando.
  2. Mtie katika oveni na muoke (bake) katika moto wa  350º-400º kwa muda wa takriban dakika 45.  
  3. Akishaiva ongezea kumpakaza tena nje na ndani sosi ilobakia na nyingine mwagia juu yake. Mwagia vitunguu, pilipili kisha mchome moto wa juu (grill)  kwa muda wa dakika 5-8 huku unamgeuza mpaka abadike rangi. Ikiwa katika jiko la makaa huku ukimgeuza na ukimpaka mafuta kidogo kidogo na mchanganyiko wa urojo wa ukwaju kwa brashi.