Pages

Ads 468x60px

Saturday, 21 April 2012

HOTELI ZA KITALII KTK FUKWE ZA ZIWA TANGANYIKA.....MKOA WA RUKWA

                               Hoteli ya kitalii iliyopo Kipili wilaya ya Nkas mkoani Rukwa
 Baadhi ya Hoteli zinazopatikana Mkoani Rukwa katika Wilaya ya Nkasi katika Tarafa ya Kipili. Boti zinazoonekana ni kwa ajili ya wateja watakaohitaji kwenda kucruise ndani ya Ziwa. Bado yapo maeneo maalum ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa Hoteli za Kitalii katika ukanda huu.
 Hakika mandhari haya yanavutia na hivyo ni baadhi ya vyumba katika Hoteli hiyo ya Kipili.
 Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Ally Kessy, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Nkasi wakimaliza ziara ya kukagua Fukwe za Ziwa Tanganyika huku wakielekea kwenye Hoteli ya Kipili ambayo kwa kiasi kikubwa hupata wageni wa kitalii.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (Kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana (Kushoto) wakiongea na watalii waliofikia katika Hoteli ya Kipili Wilayani Nkasi siku za hivi karibuni walipoenda kutembelea fukwe hizo.

Habari na picha akhsante OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA

No comments: