Pages

Ads 468x60px

Wednesday, 4 April 2012

MAMA TUNU PINDA APOKEA MICHANGO YA TAIFA QUEENS


undefinedMKE WA WAZIRI MKUU Mama Tunu Pinda leo amepokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwitikio wa ombi lake kwa Watanzania kuwaomba waichangie timu ya Taifa ya Netiboli (Taifa Queens) ili iweze kushiriki Mashindano ya Kombe la Afrika mwezi ujao.
Mama Tunu Pinda amepokea simu ya mtandao wa Zantel namba 0779-000-808 ambayo imeunganishwa na huduma ya EZY-PESA. Simu hiyo ambayo imekabidhiwa kwa uongozi wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) inawawezesha Watanzania kutuma pesa kwenye namba hii kutoka mitandao yote ya simu.
Meneja Mawasiliano wa Zantel, Bi. Awaichi Mawalla alitumia fursa hiyo kuwaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi kutuma michango yao kupitia namba hiyo ili heshima ya Tanzania ambayo imepewa jukumu la kuandaa mashindano ya Kombe ya kombe ya Africa isitetereke.
Tanzania kupitia CHANETA imepewa heshima kuandaa mashindano ya netiboli ya kombe la Afica ambayo yanatarajiwa kuanza may 8 hadi 12 mwaka huu, na gharama za kuendesha mashindano hayo ni zaidi ya milioni 120
habari Global Publisher

No comments: