Pages

Ads 468x60px

Saturday, 2 June 2012

NOELA NDIYE REDDS MISS TABATA 2012

    Redds Miss Tabata 2012, Noela Michael akipunga mkono kwa furaha baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia leo kwa kuwashinda warembo wengine 17 waliokuwa wakiwania pamoja taji hilo. Miss Tabata 2012 ilifanyika katika Ukumbi wa Dar West Park Tabata jijini Dar es Salaam na kushuhudia na mamia ya watu, huku burudani zikitoka kwa kundi la Mashujaa Musica na Mashauzi Classic.
 Redds Miss Tabata Noela Michael (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wenzake wa hatua ya tatu bora. Kulia ni mshindi wa tatu na kushoto ni Mshindi wa pili Susan Deodatus. Shindano hilo lilishirikisha warembo 18.
     Redds Miss Tabata Noela Michael (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wenzake wa hatua ya tano bora na ambao wote wamefanikiwa kupata tiketi ya kuingia katika shindano la Kanda ya Ilala, Miss Ilala 2012. Kushoto ni mshindi wa tano Filos Lemy, Mshindi wa pili Susan Deodatus, Miss Tabata, Mshindi wa tatu na mshindi wan ne, Willemina Mvungi.


Pcha na habarr thenx father kidevu

No comments: